Wednesday , 4th Nov , 2015

Producer aliyepata deal ya kutengeneza nyimbo za coke studio kutoka Tanzania Nahreel amesema hatua hiyo imempa nguvu na kumtangaza zaidi kazi zake na jina lake.

Nahreel ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kueleza kuwa kazi aliyoifanya alijua itafanya vizuri kabla hajaipeleka.

"Najisikia vizuri kwanza watu kupenda ubunifu nilioweka pale, inanipa nguvu na kuendelea kutangaza kazi yangu, jina langu kwa hiyo ninashukuru", alisema Nahreel.

Nahreal aliendelea kusema pia kuwa Coke Studio imewaunganisha wasanii wa Afrika, na kuwapa fursa ya kujifunza vitu vipya.

"Pale tunakutana na watu wengi, tunajifunza unajua hata Fid Q hajawahi kukaa na kusema mimi nitafanya kazi na Moris, kwa hiyo Coke Studio inatuunganisha na ni kitu kizuri, unajua muziki ni kujifunza kila siku kutoka kwa mwingine, kuchukua kitu fulani na kuendelea, kwa hiyo Coke Studio imetusaidia kwenye hilo zoezi la kutuunganisha pamoja watu wa Tanzania, Nigeria na Uganda", alisema Nahreel.

Pamoja na hayo Producer Nhareel amesema kwa upande wake hakukuwa na changamoto kubwa, kwani alipewa muda wa kutosha wa kutengeneza hizo kazi, hivyo ilimrahisishia.