Thursday , 7th Jan , 2016

Msanii wa bendi maarufu ya muziki nchini Cocodo Band, Remi Tone ameamua kuwapa nafasi wadau na mashabiki kuweza kughani mashairi yao katika uzinduzi wa albamu ya mashairi 'Spoken Word' inayoitwa P.O.E.M.S ya Mukimala.

Bendi maarufu ya muziki nchini Cocodo Band

Remi amesema onesho hili lililobatizwa jina New Year Poetry Party litakalofanyika leo jijini Dar es salaam litafanya onesho kupitia Open Mic kwa washairi, wanamuziki na wachekeshaji ambao wanaweza kuonesha vipaji vyao ambao wao kama bendi watazindua albamu yao hiyo mpya.

Remi ameongea na eNewz kuhusiana na nafasi yake katika bendi hiyo inayofanya vyema nchini na mipangilio ya bendi hiyo kwa mwaka huu.