Friday , 12th Jun , 2015

Bendi maarufu ya muziki nchini Tanzania inayopiga muziki wa kiafrika katika miondoko ya Afro-Pop, jumapili hii wanatarajia kutumbuiza katika gala la Sanaa la 'Nafasi Art Space' kwa ajili ya kuadhimisha siku ya Umoja wa Ulaya (Europe Day).

bendi maarufu ya muziki 'Cocodo band' ya nchini Tanzania

Cocodo ambao wanafanya vyema na wimbo wao unaoitwa 'Agwe Mwana' wimbo ambao ni soundtrack uliotumika katika filamu maarufu ya 'Sunshine' ambayo imeshirikisha mastaa mbalimbali akiwemo Ben Pol na Bi Kiroboto' wameelezea kuwa katika tukio hilo kubwa litakalofanyika jijini Dar Es Salaam, wanatarajia kutambulisha nyimbo zao mbili kwa mpigo, zikiwemo “Mdundiko” na “Imbange” ambazo zimepigwa live.

Wakali hao ambao wanaunda kundi hilo la watu tisa wote wakiwa na uwezo wa hali ya juu katika uimbaji na upigaji wa vifaa vya muziki vya Kiafrika kama ngoma, marimba na Carabashi kwa kuchanganya na vifaa kama magitaa, drums na keyboard, wameiambia eNewz kuwa ngoma hizo mbili mpya zimerekodiwa katika studio za MFDI zilizopo Masaki jijini Dar es salaam.