Akiongea na enewz Ally Choki ambaye ndiye mkurugenzi wa bendi hiyo amesema kuwa katika uzinduzi huo utakaofanyika huko Mbagala jijini Dar es Salaam, wasanii mbalimbali katika tasnia ya burudani wataisindikiza bandi yake wakiwemo bendi ya Mashujaa Musica, Malkia Khadija Kopa ‘Top in Town’, Makhirikhiri wa Bongo, Linah, Amini na wasanii wengine wengi.
Bendi ya Extra Bongo inatamba na nyimbo kama Mtenda Akitendwa, Watu na Falsafa pamoja na Ufisadi wa Mapenzi imepanga kuleta mapinduzi makubwa katika uzinduzi huo.