Friday , 1st Aug , 2014

Star mkubwa kabisa kutoka Uganda, Jose Chameleone atadondosha bonge la show katika Tamasha la 'Tubonge' litakalofanyika leo usiku ndani ya ukumbi mkali wa starehe wa Maisha Club jijini Dar es Salaam.

msanii Jose Chameleone wa Uganda

Msanii huyu mkubwa ambaye pia yupo katika orodha ya wasanii 10 matajiri zaidi Afrika, atafanya onesho hili sambamba na msanii Vanessa Mdee ambaye anafanya poa katika muziki hapa Bongo.

Mashabiki wa muziki Bongo leo watapata nafasi ya kusikia Live ngoma kali kutoka kwa Jose Chameleone zikiwemo Gimme gimme, Tubonge, Wale Wale na nyinginezo kali.

Kiingilio katika onesho hili la aina yake ni shilingi 15,000 tu kwa tiketi za kawaida na 30,000 kwa zile za VIP, Tubonge Concert inakujia kwa udhamini mkubwa wa EATV na East Africa Radio.

Usikose ni leo usiku ndani ya ukumbi mkali wa starehe wa maisha club.