Thursday , 20th Nov , 2014

Staa wa muziki kutoka Chamber Squad, Dark Master amesema kuwa ukimya wa kundi hilo ambao umeendelea kuongezeka tangu kufariki kwa msanii Ngwair ni kutokana na wao kujipanga na pia kutafuta menejimenti mpya.

msanii wa bongofleva kutoka Chamber Squad Dark Master

Dark Master amesema kuwa, kuna kazi nyingi za Chemba Squad na wanaendelea kufanya isipokuwa hawataki kukurupuka kuonyesha kuwa wapo, na sasa wanajipanga ili kupata msimamizi huyu kabla ya kutoka rasmi.