Wednesday , 4th Nov , 2015

Nyota wa muziki Bon'eye kutoka kundi la P-Unit ametoa maoni yake kuhusiana na tukio la video chafu ya DJ maarufu kutoka Kenya 'Dj Creme De La Creme' kuvuja mtandaoni na kukamata vichwa vya habari kwa sasa.

Nyota wa muziki Bon'eye kutoka kundi la P Unit

Mkali huyo aliyekuwa mstari wa mbele katika kumtetea Dj huyo amesema kuwa kitu ambacho DJ huyo amekifanya, hufanywa na kila mtu, isipokuwa tu wengi wao huwa hawajirekodi.

Bon'eye amemtaka DJ huyo maarufu kuwa na nguvu katika kipindi hiki kigumu na cha kukabiliana na maoni na hukumu mbalimbali kutoka kwa watu, akiamini kuwa ni kipindi cha mpito na hali baadaye itarejea kama kawaida.

Hata hivyo, DJ huyo ameonekana kuendelea kuwa karibu na familia yake na pia kuendelea na kazi kama kawaida, huku pia habari kuhusiana na video yake chafu zikiendelea kutawala mijadala mtandaoni.