Friday , 28th Nov , 2014

Baada ya kimya cha muda mrefu, staa wa michano Bobby Mapesa kutoka nchini Kenya, anatarajia kurudi kwa kishindo katika gemu, akiwa amewekeza kitita cha shilingi zipatazo milioni 50, katika projekti ya video yake mpya akimshirikisha mwanadada Vivian.

msanii wa muziki nchini Kenya Bobby Mapesa na Vivian

Bobby Mapesa anatarajia kuachia kazi hii kubwa tarehe 1 mwezi Desemba, na kuhusiana na suala la gharama ambazo ametumia katika kuifanya kazi hii, staa huyu amesema kuwa anachukulia kawaida kutokana na kuufanya muziki wake kama biashara ambayo anawekeza ndani yake.

Video hii mpya ya Bobby imetayarishwa na muongoza video mahiri, Kevin Bosco akiwa na rekodi ya kufanya kazi nzuri za wasanii wa hapa Tanzania, ikiwepo video ya Namchukua - Shilole, Mr Nay ya Nay wa Mitego na Mfalme ya mwana FA kati ya nyinginezo.