Friday , 9th Oct , 2015

Rapa Black Rhyno, ametoa somo kwa wasanii wenzake kutumia nafasi vizuri kutengeneza maktaba ya ngoma ambayo itaruhusu kuendelea kuwepo katika muziki bila kuishiwa hata pale ambapo itatokea wanabanwa na shughuli nyingi.

Rapa Black Rhyno wa nchini Tanzania

Rhino amesema kuwa, ingawa kuna changamoto ya mtindo wa muziki kupitwa na wakati kutokana na mtindo wa kuhifadhi ngoma, faida inabaki kubwa kutokana na kueleweka wazi kuwa, lolote linaweza kutokea na kufelisha nafasi ama uwezo wa msanii kufika studio kufanya ngoma.