Billnass ameeleza hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kupitia ukurasa wa kijamii wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia majira ya saa 8:00 mchana hadi 10:00 jioni baada ya kuonekana picha katika mitandao za kijamii zikiwaonesha wawili hao wakiwa studio katika siku za nyuma kidogo.
"Nina mahusiano mazuri na Alikiba na huwa ananishauri mambo mengi katika kazi zangu hata muda mwingine huwa tunataniana, naamini anakubali kazi zangu maana huwa nikiachia ngoma huwa ananiambia mdogo wangu hapo fresh au kazia buti sehemu fulani. Inshallah panapo majaliwa nitafanyakazi na Alikiba ila kwa sasa sitaki kuliweka wazi suala hili, ila watu wajue tu kuwa tunamawasiliano mazuri baina yetu", amesema Billnass.
Kuwa supa na Instagram ya bure toka Vodacom kwa kununua kifurushi cha kuanzia buku tu.



