Mo Music ameyasema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kuwa producer huyo amekuwa msaada mkubwa kwake mpaka kufikia alipo.
“Lolly Pop anajua uwezo wangu wa uimbaji ukoje na ananisapoti sana, bila Lolly pop nafikiri MO Music angechelewa sana kuanzia kwenye basi nenda mpaka sasa hivi, ushirikiano wake ni 90%”, alisema MO Music.
MO Music aliendelea kusema kwamba mpaka sasa bado yuko na producer huyo na anaishi nae nyumba moja, na kuongelea suala la kutoelewana msanii Baraka de Prince ambaye wote walikuwa chini ya producer huyo.
“Mimi na Baraka tupo sawa ingawa hayupo tena na Lolly Pop, na kuhusu suala la kulalamikia yeye kuwa nominated kwenye tuzo nilihoji kwa sababu ni moja ya part ya muziki wangu, lakini sikuwa na tatizo nae kabisa, na pia mimi nilikuwa mmoja wa waliopost kumuombea kura wakati wa tuzo”, alisema MO Music.
Pamoja na hayo MO Music ameongelea wimbo wake mpya wa skendo na kusema kuwa wimbo huo umefanya vizuri na kuvunja rekodi ya nyimbo zake zilizotangulia, kwa muda mchache tangu aiachie.
“Skendo naitabiria kuwa mega hit, nafikiri imevunja rekodi ya nyimbo zangu zote ndani ya masaa manne kwa sababu mimi huwa natathimini nyimbo zangu ndani ya masaa manne tangu niiachie”, alisema MO Music kwenye Planet Bongo ya EA Radio.