Big Boss
Biggie Boss amesema kuwa, ameamua safari kutoka tofauti sana na kuandika juu ya swali kubwa ambalo kila binadamu anapata changamoto ya kufahamu majibu yake, kwa kutokufahamu kesho yake itakuwaje ama sekunde chache tu kutoka wakati uliopo.
Baada ya kutafakari sana juu ya wazo hilo, msanii huyo ameamua kuwasilisha tafakari ama falsafa hii kupitia ujumbe mzito ndani ya mashairi na vilevile video ya kipekee kabisa ya ngoma yake mpya - This Time Tommorow.
Kuhusiana na kazi hii ambayo unaitazama sasa kupitia eNewz kwa mara ya kwanza kabisa, Bigie Boss anafafanua juu ya msukumo ambao umemfanya kuandika rekodi ya tofauti kama hii na vile video yake ambayo imeandaliwa kwa kiwango kikubwa katika mazingira mepesi ya ufukweni.

