Saturday , 11th Apr , 2015

Akiwa pia ni kati ya wasanii wanaofanya vizuri katika chati, staa wa muziki Belle 9 amesema kuwa, kutokuwahi kutambulika kwa kupata tuzo kwa upande wake ni kitu ambacho kimewahi kumsumbua katika kipindi cha nyuma na kumfanya ajisikie vibaya.

Belle 9

Belle 9 amesema kuwa, amekuwa akijiuliza sana juu ya vigezo vinavyomuwezesha msanii kutuzwa akikiri kabisa kuwa tuzo ina maana kubwa kwa msanii, kwa upande wake akisisitiza kuendelea kukomaa kufanya kazi kali, akitoa kauli kuwa huenda sasa ndiyo wakati wake umefika.