Wednesday , 11th Nov , 2015

Msanii wa muziki Bebe Cool wa nchini Uganda, amemrushia maneno makali DJ maarufu wa nchi hiyo, Erycom ambaye anafanya kazi zake barani Ulaya, baada ya kuudhiwa na kauli aliyotoa kumhusisha Rais Yoweri Museveni kuwa anaiongoza nchi hiyo na udikteta.

Bebe Cool

Bebe Cool katika kuonesha kuwa moyo wake upo pamoja na Rais Museveni katika kila hali wakati huu wa kampeni, amemtaja DJ Erycom kama mtu dhaifu ambaye yupo katika hali ngumu licha ya hatua yake ya kuhama Uganda kwenda kutafuta maisha bora zaidi barani Ulaya.

Mpaka sasa hakuna majibu ya muendelezo wa uhasama huo kutoka kwa Dj Erycom, wakati huu Bebe Cool akiendelea na harakati za kutumbuiza katika mikutano ya awali ya kampeni za chama tawala cha NRM nchini Uganda.

Tags: