Friday , 5th Jun , 2015

Msanii wa muziki Barnaba 'Classics' ameeleza kuwa lengo la Studio yake mpya ya High Table, licha ya kuwa inahusika na utayarishaji wa kazi za Bongofleva pekee ni kuuwekea muziki huo uhai, na kuufanya udumu zaidi ya ilivyo sasa.

Bernaba

Barnaba amesema kuwa, kwa kazi chache ambazo ametayarisha mwenyewe na zimetoka sasa, na ana imani kubwa kuwa ataweza kushindana na soko la muziki nje ya nchi.

Staa huyo amekazia kuwa, kwa feedback ambayo ameipata mpaka sasa kutoka rekodi ambazo tayari ameziachia kupitia studio yake hiyo, na kuwa uwezo alio nao katika muziki, amejiweka fiti kuja na 'sound' ambayo itauvusha muziki wa hapa nyumbani kushindani na muziki kutoka nje ya Tanzania.