Wagosi wa Kaya
Kazi za wasanii hawa ni video mbili za ngoma inayokwenda kwa jina Bao na nyingine ikiwa inakwenda kwa jina Gahawa ambazo zote zimeachiwa ndani ya siku moja, zikiwa ni kazi safi za video zilizofanywa na muongoza video mahiri Mecky Kaloka, audio zake zikiwa zimefanyika katika studios za Tongwe Records.
Wagosi wa Kaya wamefanya kazi hii maalum kwa kuwaonyesha mashabiki kuwa bado wanaiweza michano, na hii ni baada ya miaka mingi ya kila mmoja wao kujikita katika shughuli zake binafsi.
Kupitia video ya 'Bao' ambayo, wasanii hawa wamejaribu kutumia usanii wao kuzungusha maneno ili kufikisha ujumbe maalum unaowalenga wapenzi walio katika mahusino, hususan wanandoa juu ya namna ya kudumisha mahusiano yao.