Baby J
Baby J ambaye kwa sasa anaendesha muziki wake akiwa chini ya Mkubwa na Wanawe, pia akaeleza kuwa kwa roho iliyokunjuka kabisa, wasanii wenzake wanatakiwa kujifunza na kumtazama kama mfano, Vanessa Mdee staa ambaye ameweza kupiga hatua kubwa kimuziki, eNewz ikiwa na za chini ya carpet juu ya kuwepo kwa kolabo kati ya wasanii hawa wawili njiani.
Baby J anayewakilisha poa kutoka visiwa vya Zanzibar, sambamba na maneno hayo amekazia kuwa, mafanikio ya mtu ni nafasi ya kujifunza na si kukunja na kuoneana wivu, kitu ambacho kinarudisha muziki nyuma kwa kiasi kikubwa.