Saturday , 13th May , 2017

Nikki Mbishi amewasahihisha wale wanaosema kwamba hana kazi nzuri ndio maana sokoni jina lake limefifia na kusema kwamba muziki wa sasa umekuwa siyo wa tasnia bali wa familia, ndio maana wachache wanaonekana na kamwe hajawahi kuwa na kazi mbaya.

Mbishi amefunguka kwenye Planet Bongo ya East Africa radio  wakati akipiga story tatu na kusema kwamba hajawai kutoa wimbo mbaya na ndiyo maana anaendelea kudumu kwenye 'game' huku akikutana na changamoto, na kuongeza kuwa tasnia imegeuka na kuwa ya familia ndiyo sababu yeye amekuwa mwanaharakati wa kuikomboa.

Nikki amedai kwamba "Napata challenge na nnachokifanya, naonekana chizi, watu wanasema kwamba sifanyi muziki mzuri nazungumzia game. wapo wanaongea maneno mabaya sana na wengine wanakoment kwenye mitandao ya kijamii kwamba nitakuja kushtuka kuwa muziki ulikuwa unalipa nikishazeeka, mimi nawajibu sina muziki mbaya"- Nikki Mbishi.

Aidha Mbishi amezidi kufunguka na kutoa mifano kwamba kuwa na maneno ya busara hakumaanishi kutamfanya tajiri kwani kina Mandela walizungumza maneno ya busara lakini bado hawakufikia utajiri wa Billgate na ndivyo ilivyo hata kwenye mashairi yake

Msikilize Mbishi hapa chini akidadavua zaidi.