Friday , 9th May , 2014

Wasanii wa muziki wa nchini Kenya, akiwepo Anthomy Mwangi, maarufu kama Anto Neosoul, Wangechi na Just A Band, kutokana na kujituma na mafanikio makubwa katika kazi zao za muziki, wameweza kukubalika na kuvutia chombo cha habari cha kimataifa.

Anto Neosoul

Shavu hili linatarajia kuwapatia wasanii hawa nafasi ya kutambulika zaidi wao pamoja na kile wanachokifanya katika ngazi ya kimataifa, na hivyo kuongeza mashabiki wa kazi zao na kuupeleka muziki wao katika ngazi nyingine kubwa zaidi.

Wasanii hawa katika taarifa hii, wataelezea safari zao za kimuziki mpaka kufikia ngazi waliyopo sasa, na hii ni kwa lengo la kuwasaidia watu wengine kufahamu kuwa, safari kuelekea mafanikio ni kitu ambacho kipo na kinawezekana kwa kila mtu bila kujali anatokea katika mazingira duni kiasi gani.