Tuesday , 25th Mar , 2014

Mshindi wa shindano la Top Model kwa mwaka 2014 kutoka Tanzania, Mrembo Annastasia Gura amesema kuwa, kuna umuhimu mkubwa wa wadau hususan wasichana kujitokeza kwa wingi kujihusisha na masuala ya mitindo, ili kujiongezea ufahamu wa mambo.

Annastazia Gura -Tanzania Top Model 2014

Mrembo huyu ambaye ataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya dunia ya Top Model kwa mwaka huu, amesema anaona bado kuna umuhimu wa kuelimisha watu utofauti wa uanamitindo na uhuni, na kuanza kuangalia umuhimu na elimu mbalimbali ambazo zinapatikana kupitia mashindano haya.

Mwanamitindo huyu amesema kuwa, Kupitia ushiriki wake katika mashinano ya Top Model Tanzania kwa mwaka huu, ameweza kujifunza mambo mengi muhimu kuhusiana na namna ya kuwasiliana na kushirikiana na watu hususana katika mazingira ambayo wanakuwepo kwa wingi (Umati).