Thursday , 24th Dec , 2015

Msanii mkongwe wa uziki wa Dansi nchini Tanzania ambae anatamba na Bendi ya African Stars (Twanga Pepeta) Kamarade Ally Choki amesema anafunga mwaka 2015 kwa kuibuka na nyimbo za Bongofleva.

Msanii Mkongwe wa Muziki wa Dansi nchini Tanzania Kamarade Ally Choki

Ally Choki katika safari hiyo mpya, ameanza na wimbo mmoja ambao amemshirikisha Mwanamuziki Cassim Mganga alioupa jina la Caro akijipanga kuendeleza mpango na kolabo na Shilole na Ommy Dimpoz na wengine kibao ambao kolabo zao ataziweka kwenye album atakayotoa mwakani.