
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Chid Kisoki amedai kuwa chanzo kikubwa cha ugomvi huo msanii huyo ni matumizi ya unga, ambapo siku ya tukio TID alianza kumwagia pombe mwenzake.
"Mimi nilikuwa nimefiwa na baba yangu kwa hiyo nilipita eneo walilopo kama sehemu ya kupumzikia, na TID alikuwepo baada ya muda akaniomba elfu 20, ili apige mambo yake, nikamwambia sina baada ya muda akaanza kutumwagia pombe mimi nikaamua kuondoka."
"Nilipofika nyumbani nikashangaa ananifuata anaanza kunituhumu kuwa nimempiga, sijakaa vizuri tukaanza kupigana, sema tatizo yule jamaa anakula sana unga, na hilo ndiyo tatizo lake kubwa sana, anakula sana unga. na nyinyi media mnaweza kumsaidia", amesema Kisoka.
Juzi kupitia mitandao ya kijamii TID alianza kusambaza picha kwenye mitandao ya kijamii akionesha kuumia kwenye eneo la uso, akidai amepigwa.