Tuesday , 19th Jan , 2016

Nyota wa muziki Chegge ameeleza kuwa, kundi la muziki lililotikisa chati za muziki katika kipindi cha nyuma kwa upande wa Bongo Fleva, TMK Wanaume Family, lilianzia kupitia wazo ambalo wasanii hao walilipata wakiwa katika ziara nje ya nchi.

Nyota wa muziki Chegge Chigunda

Wasanii hao kwa pamoja waliweza kukonga nyoyo za mashabiki nchini kupitia albam yao maarufu iliyobatizwa jina 'Ugali' ya Sir Juma Nature.

Chegge Chigunda amesema kuwa, yeye akiwa kama moja ya wasanii ambao walishirikishwa katika ngoma za albam hiyo, wakiwa ziarani katika kipindi hicho makundi ya muziki yakifanya vizuri, wazo lilikuja na likaundwa kundi baada ya kurudi Dar es Salaam, kundi ambalo lina rekodi ya kufanya makubwa kwenye game ya Bongofleva.