Saturday , 12th Apr , 2014

Msanii wa muziki Abdu Kiba ambaye ni mdogo wa staa wa muziki Ally Kiba, amesema kuwa katika muziki wake anakubali na kumshukuru sana kaka yake huyu kwa sapoti na mchango mkubwa katika muziki anaofanya, kitu ambacho kimemsaidia kufika juu.

Abdu Kiba na Ally Kiba

Abdul Kiba amesema kuwa mchango wa kaka yake huyu ni kitu kikubwa sana kwake huku akiweka wazi kuwa, mbali na kazi yao inayokwenda kwa jina Kidela ambayo imeweza kufanya vizuri sana, wanatarajia kutoka na kitu kingine kipya kabisa hivi karibuni kwaajili ya kuendeleza burudani na harakati za muziki.

Msanii huyu ameweka wazi kuwa kazi yao mpya itatoka rasmi mwezi wa tano mwaka huu na sasa hivi wanatumia muda wao mwingi kwaajili ya kuiweka sawa sawa.