
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali, Prof. Mussa Assad (kushoto), Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe.
Katika barua hiyo, ambayo Zitto amewatumia pia maspika wote wa nchi wanachama wa CPA na wanasheria wakuu, amesema sakata hilo lilianza baada ya Prof. Mussa Assad kusema anaamini kuwa kutotekelezwa kwa ripoti anazozitoa ni kutokana na udhaifu wa Bunge.
Zitto ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Mjini, amesema maoni hayo yamemfanya Spika Ndugai kumtaka Prof. Assad kufika mbele ya kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili ahojiwe na kujieleza.
“Mimi binafsi nimeguswa na suala hili. Naomba mabunge ya Jumuiya ya Madola muingilie kati si tu kwa sababu agizo la Spika Ndugai linavunja Katiba bali pia ni hatari kwa mustakabali wa Jumuiya ya Madola kwa ujumla”, ameandika Zitto katika barua.
Ameeleza kwamba endapo CAG ataadhibiwa na Kamati ya Bunge kwa kutoa maoni, basi ni wazi kwamba uhuru wa Taasisi ya Juu ya Ukaguzi (SAI) utakuwa umevunjwa, kinyume na makubaliano yaliyofikiwa na kwenye mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Madola mwaka 2013.
Tayari barua ya Zitto imekwishapokelewa na Msaidizi wa Katib Khan, Clive Barker ambaye amemjulisha Mbunge huyo kuwa amekwishapeleka ujumbe huo kwa Katibu Mkuu.
Majibu ya Barua aliyoituma Zitto Kabwe.
Spika wa Bunge Job Ndugai alimtaka CAG Assad afike kwenye Kamati ya Maadili Januari 21 kwa ajili ya kuhojiwa kutokana na kauli yake ya kwamba bunge ni dhaifu, kwa madai kwamba kauli hiyo imelidhalilisha Bunge.