Wahitimu zaidi ya elfu kumi walioitwa katika usahili idara ya uhamiaji jana.
Wahitimu hao kutoka vyuo vikuu walionyesha wasiwasi baada ya kupewa mtihani bila kuhojiwa, ikiwa anayehojiwa ndiye mhusika au kuulizwa kitambulisho au uhakiki wa aina yeyeto ile katika usaili huo.
Habari zinasema idara ya uhamiaji iliorodhesha watahiniwa 10,816 kufanya usahili wa kuajiri wakaguzi wasaidizi wa uhamiaji nafasi 70 bila kuwepo ulinzi wa kutosha kutokana na kusanyiko kubwa la watu katika uwanja huo.
Tanzania inakabiliwa na mgogoro wa vijana wasiokuwa na ajira sambamba na nchi chache nyingine duniani.Mwaka 2012 Tanzania ilikuwa inaongoza kwa vijana kati ya umuri wa miaka 15 mpaka 24 wasiokuwa na ajira ulilinganisha na nchi nyingine 109.Katika utafiti uliofanywa na taasisi ya Restless Development mwaka uliopita unaonyesha kwamba kati ya vijana 1000 nchini kote ni asilimia 14 tu ya vijana ambao wana ajira rasmi na malipo.
Kila mwaka zaidi ya wahitimu 900,000 vijana wa Kitanzania wanaingia katika soko la ajira ambalo linatoa ajira mpya kati ya 50,000 mpaka 60,000 tu.





