Tuesday , 6th Dec , 2016

Hospitali ya taifa ya muhimbili wodi ya watoto wenye saratani imesema inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vifaa vya kuwasaidia watoto wenye saratani kupata matibabu jambo ambalo limekuwa likiathiri utendaji kazi kwa wauguzi wa wodi hiyo.

Jengo la Watoto, Hospitali ya Taifa Muhimbili.

 

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam na muuguzi mkuu wa wodi ya watoto wenye saratani wakati alipokuwa akipokea msaada wa vifaa mbalimbali vya matibabu pamoja na vyakula kwa ajili ya matumizi ya watoto hao.

Amesema wingi wa watoto wanaofikishwa katika jengo hilo nayo imekuwa ni changamoto kubwa kwa wauguzi kutokana na uchache wake jambo ambalo linaathiri pia ufanisi na utendaji kazi kwa wauguzi pamoja na wagonjwa wanaofikishwa hapo.