Moja ya transfoma ya shirika la umeme nchini Tanesco, ambayo hutumika kusambaza umeme kwa wananchi.
Tukio limetokea usiku wa kuamkia jana na kuthibitishwa na meneja wa shirika la umeme nchini Tanesco mkoa wa Ilala, mhandisi Athanasius Nangali ambaye amesema limeisababishia Tanesco hasara ya zaidi ya fedha za Tanzania shilingi milioni kumi na saba.
Mhandisi Nangali amesema kuwa takribani wateja mia moja na themanini wengi kati yao vikiwa ni viwanda vinavyotumia nishati nyingi katika uzalishaji, watakosa huduma hiyo ambapo amefafanua kuwa kabla ya kuiba mafuta na vipuri hivyo, watu hao walifungua transfoma hiyo na kuiangusha chini nankusababisha eneo lote la Ali Hamza kukosa umeme.




