Rais Mstaafu Wa awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa.
Pongezi hizo zimetolewa na Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa wakati akiongea katika mkutano wa mwaka wa bodi ya makandarasi uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake waziri wa ujenzi Dr. John Magufuli amesema kuwa makandarasi wa ndani wamechangia 40% ya ajira kwa watanzania huku makandarasi wa nje wakichangia 60% kitu ambacho kinachelewesha maendeleo kwa nchi kwani Faida kubwa wanayopata makandarasi wa nje inakwenda katika nchi zao.
Aidha waziri Magufuli amewataka makandarasi wazawa kuongeza juhudi katika kazi zao ikiwa ni pamoja na kuwekeza mitaji zaidi na Teknolojia ili washindane na makandarasi wa nje na hatimaye kusaidia taifa lipate mapato mengi zaidi ambapo itasaidia kuondoa tatizo la ajira linalowakabili vijana wengi nchini.