Friday , 3rd Jun , 2016

Wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto nchini Tanzania imesema inaendelea kuimarisha Huduma za matibabu kwa wagonjwa wanaotakiwa kupimwa vipimo vya mishipa ya fahamu pamoja na saratani kwa kutumia mashine za X-Ray

Mashine ya X-Ray

Wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto nchini Tanzania imesema inaendelea kuimarisha Huduma za matibabu kwa wagonjwa wanaotakiwa kupimwa vipimo vya mishipa ya fahamu pamoja na saratani kwa kutumia mashine za X-Ray na Ultra Sound katika hospitali za Rufaa za kanda nchini.

Hayo yamebainika katika mkutano wa Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu kutoka katika Hospitali mbalimbali nchini pamoja na nje ya nchi.

Ufinyu wa Bajeti katika Wizara za afya katika nchi nyingi za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania imechangia kukosekana kwa vifaa tiba, Machine stahiki za kufanyia vipimo kwa wagonjwa pamoja na uchache wa madaktari bingwa katika hospitali nchini.

Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) Kinawakutanisha madaktari Bingwa waliobobea katika mishipa ya fahamu inayojulikana kama wataalam wa Idiolojia kutoa mikoa mbalimbali nchini kuangazia changamoto zinazojitokeza nchini na kuathiri upimaji wa wagonjwa wanaohitaji vipimo vya X-ray.

Mganga Mkuu wa Serikali Prof.Muhamad Bakari Kambi,anasema serikali inafanya jitihada za kuhakikisha Hoaspitali za kanda nchini zinakuwa na mashine hizo muhimu ili kufanya kazi wakati wote ili kuwahudumia wananchi licha ya zingine kuharibika.

Kwa Upande Mwingine,Prof.Kambi anawataka watumishi wa sekta ya Afya kuwafanya kazi kwa kuzingatia uweledi ili kuondokana na malalamiko yanayotolewa na wagonjwa