Tuesday , 4th Nov , 2014

Baadhi ya Wananchi Wilayani Karagwe Mkoani Kagera nchini Tanzania wameyakimbia makazi yao kwa sababu ya kukwepa kuchangishwa michango kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya maabara katika shule za kata.

Moja ya Maabara za Shule ya Sekondari zinazohitajika

hayo yameelezwa na Afisa Mtendaji wa Kata ya Nyakabanga Bw. John Bigimano na kusema kuwa Wanasiasa wanaohitaji kura ndiyo kimekuwa chanzo kikubwa cha wakazi hao kukimbia michango hiyo kwa kuwadanganya kuwa Serikali imetenga fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi huo.

Bw. Bigemano ameongeza kuwa hali hiyo inafanya mapaka sasa katika Shule 19 ni shule 5 tu katika kata yake ndiyo zimeanza ujenzi wa maabara hizo ambapo kwa mujibu wa agizo la Rais hadi mwishoni mwa mwezi huu shule zote ziwe zimekamilisha ujenzi huo.

Tatizo kama hilo pia limeweza kujitokeza mkoani Mara ambapo baadhi ya wakazi wa vijiji viliyovyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, wameyakimbia makazi yao kwa kusema michango wanayochangishwa ni mikubwa sana kushinda kipato chao.