Monday , 18th Apr , 2016

Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Hassan Suluhu ameutaka uongozi na Wafanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kufanya kazi kwa weledi na huruma ili kuboresha huduma ya afya Hospitalini hapo.

Makamu wa rais Samia Hassan Suluhu akiwafariji wagonjwa alipotembelea Hospitali ya Mkoa wa Morogoro

Akiongea na Watumishi wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro amewaambia wafanyakazi kuwa watambue kazi hiyo ni wito na wameichagua wenyewe hivyo hawana budi kuifanya kwa moyo wote.

Aidha, Makamu wa Rais Bi. Samia amesema kufuatia Changamoto zinazoikumba hospitali hiyo serikali italifanyika kazi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa upanuzi wa hospitali ili kuboresha huduma ya afya kwa Mkoa wa Morogoro.

Mhe.Suluhu yupo Mkoani Morogoro kwa ajili ya uzinduzi wa mbio za Mwenge unaotarajiwa kuwashwa hii leo kwa ajili ya kuzunguka nchi nzima katika kufungua miradi mbalimbali ya kimaendeleo.

Sauti ya Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Hassan Suluhu