Mafundi wakiendelea na kazi ya kuunganisha mabomba ya maji eneo la Kiluvya jijini Dar es salaam.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa shirika hilo Bw. Ibrahim Kabole jana wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam wakati akiongelea mikakati ya shirika hilo katika maadhimisho ya wiki ya Maji barani Afrika.
Katika Maadhimisho hayo ambayo kilele chake ni siku ya Ijumaa ambayo yanafanyika Tanzania amesema wameweka mikakati ya kusaidia kufikia malengo ya kumwezesha kilwa mwananchi barani afrika kupata maji safi na salama.
Amesema kuwa zaidi ya waafrika milioni 700 ambao ni sawa na asilimia 50 hawana vyoo safi na salama na hatua hiyo inaweza kuleta madhara kwa afya na usafi wa mazingira.
Bw. Kabole ameongeza kuwa wengi ambao hawajafakiwa na huduma hizo ni wasio na uwezo, wakiwemo wazee,walemavu na wanaoishi maeneo ya vijijini na kusema kuwafikia kunahitaji ushirikiano wa pamoja.





