Waziri Ummy Mwalimu akiongea na wazee wanaotunzwa katika kituo cha Kilima wilayani Bukoba, alipowatembelea
Rai hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu mara baada ya kuwatembelea wazee waishio kwenye makazi ya wazee wasiojiweza Kilima iliyopo Bukoba vijijini.
Waziri Ummy amesema watanzania wengi hivi sasa hawafuati maadili ya kitanzania na utamaduni wa kusaidiana pale mtoto anapofiwa na wazazi au asiye na uwezo na kumsaidia.
"Unapoona mtoto ana matatizo ni vyema kujitolea kwa kumlea kuliko kumuacha akiteseka, mzazi anajijali yeye na watoto wake pekee, mtu anatupa chakula na nguo badala ya kuja kuwafariji wazee hawa, ndiyo imani na dini zetu zinavyotuambia" alisisitiza
Suala la kuwatunza wazee sio la serikali peke yake, mila za kitanzania ni kusaidiana "mtoto wa mwenzio ni wako", hivyo jamii kujenga utaratibu wa kutembelea makazi ya wazee wasiojiweza ni baraka kwa familia.
Aidha, ametoa wito kwa ndugu na jamaa wenye wazee kwenye makazi yote nchini kuwachukua na kuwalea ili waepukane na adha zilizopo huko.
Kwa upande wa matibabu bila malipo kwa wazee, Waziri Ummy ametoa agizo kwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuwapatia vitambulisho vya bima ya afya kwa wazee wote kumi na saba waishio kwenye makazi hayo.
Naye mzee aishiye kwenye makazi hayo John Lwiza alimuomba waziri huyo kuwasaidia chombo cha usafiri kuweza kurahisisha kuwapeleka hospitali mara wanapougua



