Takwimu hiyo imetolewa na wakala wa vyuo vikuu nje ya nchi ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link Bw. Abdulmalik Mollel alipokuwa akiongea na waandishi wa habari hii leo jijini Dar es Salaam kwamba kumekuwa na mwamko wa watanzania kujiendeleza kielimu katika vyuo vya India, Ukraine, Canada, Urusi na Marekani.
Mollel amesema, Global Education Link imeandikisha wanafunzi 250 ndani ya mwezi Juni na Julai pekee idadi ambayo amesema inaongezeka kutokana na ada za masomo ya udaktari kwa nchi ya India kufanana na ile ya vyuo vya ndani ya nchi, huku kukiwa na utofauti mkubwa wa wataalamu, vifaa vya kufundishia na ubora wa elimu.
Aidha, Bw. Mollel, ameishauri serikali kupitia Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi nchini kuingia mkataba na vyuo vya nchini India vyenye ubora wa elimu ili kupata wataalam waliobobea katika taaluma ya udaktari na uhandisi kwani vyuo vya ndani vimekuwa vikidahili idadi ndongo ya wanafunzi kuliko wingi wao jambo ambalo linapelekea kila mwaka kuwepo na upungufu wa wataalam wa udaktari.



