Monday , 5th Oct , 2015

Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakari Zuberi Ali amesema mpaka sasa ni watu 8 ndio wameripotiwa kufa katika tukio la mahujaji kukanyagana huko makka nchini Saudi Arabia wakati wa Swala ya hijja,

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mufti Zuberi ameongeza kuwa juhudi zinaendelea kufanywa kwa pamoja kati ya balozi wa Tanzania na Serikali ya Saudi Arabia kujua idadi kamili ya Watanzania waliokwenda, waliofariki, waliopotea na waliofanikiwa kurudi.

Hata hivyo Mufti Zuberi amesema kuwa mwaka huu hakutakuwa na shamra shamra za kuwapokea mahujaji wanaorudi toka makka sababu ya kuomboleza msiba huo.

Aidha Mufti Zuberi amesema chanzo cha ajali ni baada ya kufungwa kwa njia moja ya kwenda katika eneo la jamarati ili kumpiga mawe shetani na hivyo kusababisha watu kuwa wengi zaidi ya uwezo wa njia.