
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya hiyo, John Haule amesema watanzania hao bado hawajanyongwa kutokana na serikali ya China kuthamini ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na China na huenda wakabadilishiwa kifungo na kufungwa kifungo cha maisha jela badala ya Kunyongwa.
Haule amesema serikali ya Tanzania itahakikisha inadumisha ushirikiano na China kwa lengo la kupatikana kwa fursa za kiuchumi na kwamba tayari serikali ya China imetoa vifaa kwa Tanzania kwa ajili ya kugundua watu wanaosafirisha dawa za kulevya katika viwanja vya ndege.