Tuesday , 7th Jul , 2015

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, amemtaka Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Juma Idd kutengua kauli aliyoitoa mwishoni mwa wiki kuwa endapo ikibainika kuna mwananchi amejiandikisha katika kata asiyoishi atakatwa jina lake.

kurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha Juma Idd

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, amemtaka Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Juma Idd kutengua kauli aliyoitoa mwishoni mwa wiki kuwa endapo ikibainika kuna mwananchi amejiandikisha katika kata asiyoishi atakatwa jina lake.

Akizungumza jana ofisini kwake na waandishi wa wahabari, amesema kuwa yeye ni kiongozi aliyechaguliwa na wananchi na hatishwi na kauli zinazotolewa mkurugenzi huyo, kwani zinalengo la kuwaogopesha wananchi wasiopata fursa ya kujiandikisha kwakutumia BVR.

Amesema Idd hawezi kuwazuia wananchi wasijiandikishe katika kata nyingine, lakini pia hakuna sheria inayowaruhusu Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kuwakata wananchi majina kwa madai ya kuwa hawawatambui.

Lema amesema tayari amekusanya majina ya wananchi, ambao zaidi ya 8,900 walioachwa kuandikishwa kwenye Kata 12, ambazo tayari zoezi hilo lilishafanyika na kusisitiza kuwa wananchi hao, wanajipanga kwenda kwa mkurugeni huyo, kudai haki yao ya msingi na kikatiba.

Lema ametaja wananchi walioachwa bila kujiandikisha wanatoka katika Kata ya Olasiti, Ungalimited , Sokon 1 na Sinoni na bado anaendelea kukusanya majina ya wananchi, katika kata zote ambazo hawajaandikishwa.

Naye Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha Juma Idd alipopigiwa simu ya kiganjani amesema, sheria inasema kila mtu ajiandikishe mahali anapoishi ,lakini Lema hakuwa katika Baraza wakati likivunjwa, yawezekana alichoambiwa amekitafsiri vibaya, lakini alisisitiza sheria inasema mwananchi anapaswa kujiandikishamahali anapoishi.

Awali mwishoni mwa wiki wakati wa kuvunja Baraza la Madiwani wa Jiji la Arusha, Idd alisisitiza madiwani kuwa, wananchi wa Kata husika wajiandikishe katika daftari la kupigia kura kwenye maeneo yao, vinginevyo siku ya kupiga kura watahakikiwa na wenyeviti wa serikali ya mitaa na hawataruhusiwa kupiga kura.