Friday , 10th Jun , 2016

Serikali imesema wasichana 500 wanatumikishwa katika kazi hatari zikiwemo za ukahaba katika nchi za Asia na Uarabuni baada ya kusafirishwa na mtandao unaojihusisha na kzi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa za wasichana hao huahidiwa kupelekwa huko kwa lengo la kufanya kazi za ndani lakini wanapofika katika nchi hizo hutumikishwa ikiwa ni pamoja na kuhutumikishwa kwenye biashara ya ngono.

Watu wanaohusika katika kazi ya kuwatafuta wasichana hutafuta wenye umri kati ya miaka 18 na 24 na hata chini ya umri huo na kuwalaghai kuwa kuna fursa za ajira katika mahoteli, migahawa, maduka makubwa au kazi za nyumbani nchi za nje na kuwaahidi kuwagharamia gharama za kwenda huko pamoja na vibali vinavyotakiwa.

Baada ya kufika huko hunyang’anywa hati za kusafiria ili wasiweze kutoroka na kulazimishwa kujiingiza katika biashara za ukahaba ili kurejesha gharama za kuwasafirisha kutoka Tanzania kwenda katika mataifa hayo.

Aidha taariza zinasema kuwa wasichana wengi wamekuwa wakikimbilia katika Balozi za Tanzania kuomba kurudishwa nyumbani .

Chanzo BBC.