Friday , 20th Nov , 2015

Waliokuwa wasambazaji wa bidhaa katika maduka ya Uchumi jijini Dar es Salaam ambayo kwa sasa yamefungwa wameiomba serikali kuingilia kati

Waliokuwa wasambazaji wa bidhaa katika maduka ya Uchumi jijini Dar es Salaam ambayo kwa sasa yamefungwa wameiomba serikali kuingilia kati ili waweze kulipwa fedha zao ambazo wanadai kwa mujibu wa bidhaa walizopeleka katika madukani hayo na mpaka sasa hawajalipwa.

Wakiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana wasambazaji hao wamesema wamekuwa wakisumbuliwa na mabenki kutokana na fedha walizonunulia bidhaa hizo zilitokana na mikopo kwa mategemeo ya kulipwa ili waweze kurejesha mikopo hiyo katika benki husika.

Wasambazaji hao zaidi ya mia mbili wamesema wanalazimika sasa kusitisha biashara zao kutokana na kukosa mitaji huku wakiwa na tishio la kutaifishiwa mali zao na taasisi za fedha kutokana na mikopo waliyochukua.