Friday , 5th Feb , 2016

Wanawake wajasiriamali wa kitanzania wanaofanya biashara katika maeneo ya mipakani wameiomba serikali kufungua fursa za kibiashara katika nchi hizo , ili kukabiliana na ushindani uliopo wa kibiashara.

Mkurugenzi Mtendaji Msaidizi kutoka Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya kuwasaidia wanawake wajasiriamalia wanaofanya biashaara mipakani (TWCC),Bi. Mwajuma Hamza

Wanawake hao wamesema kuwa kuwezesha huko kutasaidia kukuza uchumi wao na kuondokana na umasikini kwa kupunguza tozo za kodi kwa kuwa ndiyo sababu kubwa inayowafanya wajasiriamali wengi kupita njia za panya

Wanawake hao wajasiriamali kutoka mikoa kumi na tano na maeneo mbalimbali ya mipakani mwa Tanzania wamesema hayo jijini Arusha katika ziara ya kujifunza kutoka kwa wanawake wezao waliyofanikiwa kibiashara .

Wamesema licha ya kujionea mafanikio makubwa yaliyofikiwa bado serikali inapaswa kuondoa vikwazo vinavyowakabili katika maeneo ya mipakani, hali inayolazimu kutumia njia za panya kukwepa ulipaji wa kodi ..

Mkurugenzi Mtendaji Msaidizi kutoka Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya kuwasaidia wanawake wajasiriamalia wanaofanya biashaara mipakani (TWCC), Bi. Mwajuma Hamza amesema katika mradi huo wanawazesha wanawake hao kuweka kufanya biashara mipakani na kutambua biashara za kuvuka mipaka.

Kwa upande wake Juna Molel ni mjasiriamali aliyefanikiwa katika biashara ya mitindo ya mavazi mbalimbali ya kiafrika kwa upande wake anasema siri ya kufanikiwa katika biashara ni kuzalisha bidhaa zenye ubora ili kuweza kushindana katika soko la Afrika Mashariki na kufanya tafiti kabla ya kuzalisha bidhaaa.