Tuesday , 15th Sep , 2015

Kampuni ya Stamigold mkoani Kagera imeanzisha huduma ya upimaji wa saratani ya kizazi na utoaji tiba bure kwa akina mama waishio katika vijiji jirani vinavyo uzunguka mgodi huo ili kuweza kunusuru maisha yao.

Mtaalamu kutoka Taasisi ya uzazi na malezi bora (UMATI) Tawi la Mwanza Dkt. Milka Eyembe

Akina mama ambao wamepata huduma hiyo wamesema kuwa ni mara yao ya kwanza kupata huduma hiyo huku wengine wakidai kutumia gharama kubwa za usafiri na matibabu kufuata huduma hizo katika hospitali kubwa hali ambayo huwafanya washindwe kupima mara kwa mara.

Aidha kuanzishwa kwa huduma hiyo kunaungwa mkono na baadhi ya akina baba wa vijiji hivyo huku wakiomba ushirikiano udumishwe kati ya kampuni ya stamigold na wananchi ili kuleta mabadiriko na kukuza uchumi ndani ya vijiji vyao.

Akiongea baada ya kukamisha zoezi la upimaji katika vijiji hivyo mtaalamu kutoka taasisi ya uzazi na malezi bora (UMATI) Tawi la Mwanza Dkt. Milka Eyembe amesema kuwa wameamua kutoa huduma baada ya ugonjwa huo kuhatarisha maisha ya akina mama huku akiwasisitiza kuhudhulia vipimo mara kwa mara ili iwe rahisi kuzuia maambukizi kabla ugonjwa haujaleta madhara.

Kwa upande wake meneja wa kampuni hiyo amesema kuwa utoaji wa huduma ya Afya kwa wanyafakazi ni utaratibu wao huku akibainisha zoezi hilo litakuwa endelevu kwa wananchi walio jirani na mgodi huo ili kuweza kupunguza gharama za matibabu walizokuwa wakizitumia kufuata huduma hiyo.