
Akiongea leo Jijini Dar es Salaam, Daktari wa Afya ya Uzazi kwa baba, mama na mtoto Dkt. Ali Mzige amesema katika aina za saratani mia moja zilizopo duniani, asilimia 85 ya vifo vya saratani nchini kwa wanaume inasababishwa na uvutaji wa Tumbaku.
Dkt. Mzige amesema mpango wa serikali kuanza chanjo kwa wasichana walio na umri wa miaka tisa utasaidia kupunguza kiwango cha vifo vya saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake.