
Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Dkt Shukuru Kawambwa
Waziri wa wizara hiyo Dkt Shukuru Kawambwa ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam, kufuatia kile alichadai kuwa ni uwepo wa dhana potofu kuwa serikali imeyapika matokeo ya kidato cha nne ya mwaka jana kwa lengo la kujisafisha kwamba imekuwa ikifanikiwa katika kuboresha kiwango cha elimu.
Waziri Kawambwa amefafanua kuwa kupitia mpango wa matokeo makubwa sasa, BRN serikali imefanikiwa kufanya mageuzi ya haraka katika sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kufanikiwa kuongeza ufaulu wa masomo katika shule mbalimbali.