Thursday , 19th May , 2016

Wananchi wa kata ya Madimba, halmashauri ya wilaya ya Mtwara, wametakiwa kushiriki kikamilifu zoezi la kufyatua Matofali lililolenga kutatua changamoto mbalimbali za miundombinu ya elimu zikiwamo nyumba za walimu na vyumba vya madarasa.

Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego na Mbunge wa Mtwara Vijijini. Mhe. Hawa Ghasia.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, alipotembelea katika shule ya sekondari ya Madimba kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazoikabili shule hiyo, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku tano anayoifanya mkoani mwake.

Dendego amemwagiza Mwenyekiti wa kijiji cha Madimba, Mohamed Madiva, awahamasishe wananchi wake ili watekeleze zoezi hilo kwa haraka ili kutatua tatizo la uhaba wa nyumba za walimu ambalo linawakabili walimu wa shule hiyo ambao wengi wao ni wageni kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini.

Mkuu wa shule hiyo, Ahmad Kwerendu, ameomba ushirikiano udumishwe baina ya uongozi wa shule, jamii pamoja na viongozi wa ngazi za juu ili kuweza kumaliza changamoto zilizopo.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego