Sunday , 30th Nov , 2014

Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, wamepongeza maazimio ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya viongozi wote wa serikali waliohusika na kashfa ya uchotwaji fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.

Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo

Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, wamepongeza maazimio ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya viongozi wote wa serikali waliohusika na kashfa ya uchotwaji fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.

Jana usiku bunge lilihitimisha mjadala wa kashfa hiyo na kupitisha maazimio nane likiwemo la kutaka kutenguliwa nyadhifa zao Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka, Mwanasheria Mkuu Frederick Werema na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakimu Maswi.

Wengine waliowajibishwa pamoja na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) na kuwavua nyazifa zao wenyeviti watatu wa kamati za kudumu za Bunge.

Wenyeviti waliovuliwa nyadhifa zao ni Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Victor Mwambalaswa, Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, William Ngeleja na Kamati ya Bajeti, Andrew Chenge.

Victor Mwambalaswa ametakiwa kuadhibiwa kwa kuwa ni mjumbe wa Bodi ndani ya Bodi ya TANESCO mbali ya kuongoza kamati inayohusika na suala la Nishati lenye mahusiano ya moja kwa moja na sakata la akaunti ya Tegeta Escrow.

Tags: