Wapiganaji hao wa Al-Shabab walishambulia kambi ya jeshi la Umoja wa Mataifa nchini Somalia na kuna ripoti kuwa wanajeshi kadhaa wa Kenya waliuawa huku wengine wakijeruhiwa.
Kenya imekaririwa kuwa haitaondoa wanajeshi wake Somalia hadi pale kundi hilo la al shabaab litakaposambaratishwa kabisa na amani kurejea nchini humo.
Tangu mwaka wa 2011 wakati Kenya ilituma wanajeshi wake nchini Somalia, kundi hilo limefanya mashambulio kadhaa ya kigaidi nchini Kenya na kusababisha maafa makubwa.
Chanzo BBC.

