Hii ni moja ya tukio la juzi la moto katika shule ya sekondari Lowassa iliyopo Monduli.
Akizungumza eneo la tukio hilo mwandishi wa ITV/Radio One Khalfan Khalfan Lihundi, amesema mali zote za wanafunzi zimeteketea kwa moto wakati wa usiku huku wanafunzi wakiwa kwenye masomo ya ziada hivyo madhara kwa wanafunzi hakuna.
Kwa upande wake mwalimu Florence Laurian amesema chanzo cha moto bado hakijafahamika ila yawezekana ni shoti ya umeme au ni hujuma kwa sababu moto huo kama ungekuwa ni shoti ya umeme bweni hilo linaunganishwa umeme na bweni lingiine hivyo kama ingikuwa ni shoti yote yangelipuka kwa moto.
‘’Inawezekana chanzo cha moto huu ni hujuma kwa sababu bweni hili linachukua umeme kutoka kwenye bweni lingiine ambalo linaunganishwa na mita moja lakini wakati moto unawake bweni linguine taa zilikuwa zinawaka’’ Amesema Mwl. Florence.
Aidha katika kipindi kisichozidi siku mbili shule ya Lowassa Sekondari iliyopo wilayani Munduli ilikubwa na tukio la moto wakati wanafunzi wakiwa kwenye masomo ya ziada usiku na moto ukiwa umeanzia kwenye mlango huku chanzo cha moto huo pia kikiwa bado hakijafahamika.








