
Hayo yamebainishwa katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari kuhusu tathmini ya bomoa bomoa na athari zake jijini Dar es salaam.
Kikao cha tathmini hiyo kilijumuisha mawaziri watatu Waziri wa ardhi nyumba na makazi William Lukuvi,Waziri wa nchi ofisi ya rais TAMISEMI George Simbachawene na Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais Januari Makamba.
Taarifa ya kikao hicho inaeleza kwamba bomoa bomoa itaendelea kwa wale ambao wapo katika kingo za mto msimbazi na wale wote ambao wapo hatarini wakati wa mvua.
Pia taarifa inaeleza kuwa kwa wote ambao wana hati za kukaa kwenye maeneo yao na ambao wana umiliki halali wa maeneo yao watatafutiwa maeneo mengine baada ya serikali kuridhika kama maeneo yao wapo kihalali na walipewa hati kisheria.
Hata hivyo Serikali imesema inaheshimu amri ya mahakama ya kutaka kusitishwa kwa zoezi huilo lakini watahakikisha kesi iliyopo mahakamani inashughulikiwa kwa wakati ili zoezi liendelee
Aidha serikali imesema haitavunja hoteli zilizojengwa zamani ambazo zipo katika fukwe maeneo ya Masaki badala yake wamewataka wamiliki wa hoteli hizo kuhakikisha wanalinda mazingira.