Wakulima wakiwa wanapakia viazi katika vifungashio kwa ajili ya kupeleka Sokoni.
Hapo jana wafanyabiashara wa viazi na madalali mkoani Njombe wameapa kutoendelea kununua zao hilo kutokana na vitendo vya kutoza faini vinavyofanywa nawakala aliyewekwa na mkuu wa wilaya pamoja mawakala wa vipimo kutoka mkoani iringa kwa kila anayebainika kushona viazi kwa aina ya rumbesa
Wafanyabiashara hao wamelani vikali kitendo cha wakala wa mkuu wa wilaya Baton mwapinga kutumia jeshi la polisi kuwapiga mabomu wafanyabiashara na madalali wanapotaka kujua kwanini wanakamatwa ili hali suala hilo la lumbesa ni jambo la kitaifa
Edwin Mwanzinga mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe na diwani wa kata ya Matola Halmashauri ya mji wa njombe anasema zoezi hilo linafanyika kwa maamuzi ya watu wachache ambao wanamaslahi kwa kuwa madhara ni makubwa kwa wananchi wanaolima kwa gharama kubwa na ndio wahanga kutokana na wafanyabiashara kughasiwa na serikali ya mahala husika
Lakini cha kujiuliza kwanini sheria inakazwa kwa mkoa wa njombe pekee ili hali nchi nzima lumbesa inafanyika na inauzwa katiaka masoko jijini Dar es Salaam anasema huo ni mradi wa vigogo Wachache kujinufaisha kupitia lumbesa mkoani Njombe huyu hapa tena mwanzinga
Wakulima Wanaowakilishwa bi Ema Mligo mkulima kutoka uwemba wanataka lumbesa iendelee kutumika kwa kuwa wanaona ndio kivutio cha wateja kutoka mbali wakipingana na mshono wa mfuto ambao ni kilo miamoja kuwa unapelekea viazi kutoka mkoani njombe kukosa soko
Juhudi za kuwatafta mawakala wa vipimo kutoka mkoani njombe kuzungumzia zoezi hilo zimeshindikana kutokana na mawakala hao kueleza wanaelekea vijijini kufuatilia waharifu wa rumbesa
kwa upande wake kamanda wa polisi mkoa wa njombe alipofuatwa na waandishi kuzungumzia sababu za kutumia mabomu na risasi pamoja na kuwashikilia baadhi ya madalali amesema kuwa yuko mapumziko licha ya kukiri kuwa na taarifa.